Kusaidia familia kuwa viongozi katika mazungumzo kuhusu elimu jumuishi
Guide
Imeandaliwa kwa michango ya makundi ya kifamilia kutoka kote duniani, zana hii inatoa nyenzo, mikakati na mwongozo wa kuimarisha juhudi za utetezi na kuhamasisha ushirikiano kati ya familia, walimu na watunga sera.
Inawalenga familia za watoto wenye ulemavu wa akili, pamoja na mashirika na washirika wanaounga mkono utetezi wa elimu jumuishi katika ngazi ya jamii.
Kupitia rasilimali hii, familia zinaweza kuchukua hatua kwa uelewa zaidi ili kuimarisha mifumo ya elimu jumuishi na kuhakikisha kwamba watoto wote wanapata fursa ya kujifunza na kukua pamoja.
Je, inajumuisha nini?
- Kujenga maono: Rasilimali za kusaidia familia na jamii zao kufikia uelewa wa pamoja kuhusu elimu jumuishi.
- Zana za utetezi: Mikakati ya kushinda changamoto, kutetea haki za wanafunzi na kushirikiana na shule na serikali.
- Mwongozo wa vitendo: Hatua za kufuatilia maendeleo na kushinikiza mifumo ya elimu kutekeleza majukumu yake.
- Tajiriba za familia: Ushuhuda wa kweli kutoka kwa makundi ya kifamilia nchini Kenya, Benin, Nikaragua na Peru.
Unaweza kupata ripoti na zana kamili kwa kubofya kitufe cha “Pakua” hapa chini. Pia, unaweza kupakua zana moja moja hapa.